1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

Rais wa Misri kuapishwa leo kwa muhula wa tatu madarakani

Tatu Karema
2 Aprili 2024

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ataapishwa leo kwa muhula wa tatu madarakani katika majengo mapya ya bunge yaliojengwa nje ya mji wa Cairo. Haya yamethibitishwa jana na gazeti la serikali la Al-Ahram

https://p.dw.com/p/4eK16
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi  akizungumza wakati wa kongamano la uwekezaji la G20
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi Picha: John Macdougall/AP Photo/picture alliance

Sisi mwenye umri wa miaka 69 na ambaye ameiongoza Misri kwa zaidi ya muongo mmoja, ataanza muhula wake mpya uongozini kesho Jumatano, zaidi ya miezi mitatu baada ya kuchaguliwa tena kama rais wa nchi hiyo kwa asilimia 89.6 za kura dhidi ya wagombea wengine watatu wasiokuwa maarufu.

Muhula mpya wa uongozi wa Sisi unatarajiwa kuwa wa mwisho

Mustafa Bakri, mbunge mwenye ushirikiano wa karibu na mamlaka nchini Misri, amesema kulingana na katiba, muhula huu mpya wa miaka sita, unatarajiwa kuwa wa mwisho kwa uongozi wa Sisi na kuongeza kuwa huenda serikali ikajiuzulu baada ya kuapishwa kwake kuwezesha kufanywa mabadiliko katika baraza la mawaziri.

Misri inakabiliwa na changamoto si haba

Kuapishwa kwa Sisi kunakuja wakati ambapo taifa hilo linakabiliwa na mzozo mbaya wa kiuchumi,kuongezeka kwa mfumuko wa bei na uhaba wa sarafu za kigeni unaodumaza biashara ya kimataifa.