1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

Umoja wa Ulaya waipatia Misri msaada wa dola bilioni 8

17 Machi 2024

Umoja wa Ulaya umetangaza kutoa msaada wa dola bilioni 8 kwa Misri inayokabiliwa na matatizo ya kiuchumi na migogoro katika nchi jirani.

https://p.dw.com/p/4dpAZ
Misri I Viongozi wa EU wakiwa na rais al-sisi mjini Cairo
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi mjini CairoPicha: Dirk Waem/Belga/picture alliance

Jambo hilo linalohofiwa huenda likasababisha ongezeko la idadi ya wahamiaji watakaoingia barani Ulaya. Makubaliano hayo yamepangwa kusainiwa leo wakati wa ziara ya Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na viongozi wa mataifa ya Ubelgiji, Italia, Austria, Cyprus na Ugiriki.

Rais Abdel Fattah el-Sissi wa Misri amekutana kwa nyakati tofauti na von der Leyen pamoja na Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo, ambaye nchi yake ndio kwa sasa inashikilia urais wa zamu wa Umoja wa Ulaya.

Soma pia: Umoja wa Ulaya kuimarisha uhusiano na Misri kwa kutoa ufadhili wa mabilioni dola

Mpango huo unalenga kuimarisha ushirikiano katika sekta za nishati mbadala, biashara na usalama. Fedha hizo zitatolewa kama misaada, mikopo na ufadhili mwingine katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.