1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya Magharibi kuondoa vikosi vyake Afrika magharibi?

Josephat Charo
27 Septemba 2023

Ufaransa itawaondoa wanajeshi wake kutoka nchini Niger kufikia mwisho wa mwaka huu kufuatia mapinduzi ya kijeshi katika nchi hiyo, ambayo yalikuwa pigo kubwa kwa ushawishi wa Ufaransa katika eneo la Sahel.

https://p.dw.com/p/4Wqaj
Waandamanaji wakiwa wamebeba picha iliofananishwa na rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa kwenye pambano la ndondi na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Waandamanaji wakiwa wamebeba picha inayofanana na rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa kwenye pambano la ndondi na rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Ousmane Makaveli/AFP/Getty Images

Niger, mshirika muhimu wa nchi za Magharibi katika mapambano dhidi ya uasi wa wanamgambo wa kiislamu katika eneo la Sahel, imewakaribisha wanajeshi wa nchi kadhaa za kigeni.  

Ufaransa ina vikosi 1,500 nchini Niger, vikisaidiwa na ndege zisizorushwa na rubani na ndege za kivita.

Ilikuwa na vikosi vya kupambana an uasi Afrika Magharibi kwa muongo mmoja, lakini ikaigeukia Niger kuwaweka idadi kubwa ya wanajeshi wake kufuatia mapinduzi ya kijeshi katika nchi jirani za Mali na Burkina Faso mnamo 2021 na 2022 mtawalia.

Utawala wa kijeshi uliomuondoa madarakani rais wa Niger, Mohamed Bazoum, mnamo Julai 26 umefuta mkurururo wa mikataba ya kijeshi na Ufaransa. 

Soma pia:Marekani inasitisha misaada nchini Gabon na baadhi ya misaada nchini Niger kufuatia mapinduzi ya kijeshi

Kabla mapinduzi hayo, Ufaransa ilipania kuepusha ukosoaji ambao ungejitokeza kuhusu jukumu lake katika eneo la Sahel na kupunguza kauli na fikra za kuipinga Ufaransa.

Hilo lilifuatiwa na kubadilisha muelekeo wake na kuvisaidia vikosi vya nchi za eneo hilo badala ya wanajeshi kutoka nchi za Magharibi kufanya kazi kubwa katika uwanja wa vita. 

Ufaransa ingali ina kambi zake za kijeshinchini Chad, ambako kuna vikosi 1,000, Ivory Coast vikosi 900, Senegal vikosi 350, na Gabon vikosi 400.

Baadhi ya kambi hizi zinageuzwa kuwa operesheni za pamoja na majeshi ya mataifa hayo, kupunguza jukumu kubwa la Ufaransa. 

Marekani na Ujerumani kuondoa wanajeshi wake?

Marekani ina vikosi vyake takriban 1,100 nchini Niger ambako jeshi la Marekani linaendesha harakati zake katika kambi mbili.

Mnamo 2017 serikali ya Niger iliridhia matumizi ya ndege zisizoendeshwa na rubani za Marekani kuwalenga na kuwashambulia wanamgambo.

Wanajeshi wa Mali wakiwa katika doria
Wanajeshi wa Mali wakiwa katika doriaPicha: Souleymane Ag Anara/AFP

Haijabainika wazi kiwango ambachoMarekani imetoa kama msaadawa usalama. Ubalozi wa Marekani mjini Niamey mwaka 2021 ulisema wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon na wizara ya mambo ya nje zilikuwa zimeipa Niger zaidi ya dola milioni 500 kwa ajili ya vifaa na mafunzo tangu mwaka 2012.

Kufikia Septemba 20, Ujerumani ambayo inawaondoa wanajeshi wake waliokuwa nchini Mali wakihudumu katika tume ya amani ya Umoja wa Mataifa, MUNISMA.

Ilisema vikosi 887 wangali bado wako Mali wakiwemo 755 katika mji wa kaskazini wa Gao, na wengine katika mji mkuu, Bamako.

Soma pia:Ufaransa imetangaza kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger baada ya mvutano mkali tangu kulipofanyika mapinduzi ya kijeshi

Kiasi vikosi 110 vya Ujerumani viko katika mji mkuu wa Niger, Niamey.

Italia ilikuwa na wanajeshi wapatao 300 nchini Niger kabla mapinduzi, kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya nchi hiyo.

Mnamo Agosti 6, wizara ya ulinzi ya Italia ilisema wanajeshi wake 65 walikuwa wameondoka Niger kutumia ndege ya kijeshi, wakati ilipotaka kutoa nafasi katika kambi yake ya kijeshi kwa raia ambao huenda wakahitaji msaada.

Hii iliwaacha vikosi 250 wakiendelea kuhudumu katika operesheni ya kupambana na uasi na katika ujumbe wa kutoa mafunzo ya kijeshi Niger.

Umoja wa Ulaya una vikosi kati ya 50 na 100 wanaohudumu kwa miaka mitatu katika tume ya mafunzo ya kijeshi iliyoianzisha nchini Niger mnamo Desemba mwaka uliopita kuisaidia nchi hiyo kuboresha uratibu wake na miundombinu. 
 

Ufafanuzi:Kwanini Niger ni muhimu kwa mataifa ya magharibi?