1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

RSF wakaribisha wito wa utulivu wakati wa Ramadhan

Lilian Mtono
10 Machi 2024

Wanamgambo wa RSF nchini Sudan wamekaribisha wito wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kusitisha uhasama wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

https://p.dw.com/p/4dMAA
Sudan ilipogubikwa na moshi kufuatia mashambulizi ya makombora
Moshi ukifuka wakati wa mapigano kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF, Aprili 21, 2023 wakati wa sikukuu ya Eid El Fitri. Hivi sasa RSF wanataka usitishwaji mapigano wakati wa mfungo wa Ramadhan.Picha: AA/picture alliance

Wanamgambo hao wa RSF wameahidi kusimamisha mapigano yaliyodumu kwa miezi 11. Mwezi mtukufu wa Ramadhan unatarajia kuanza Jioni ya leo Jumapili.

Kwenye taarifa yake, RSF wameelezea matumaini kwamba azimio la Baraza la Usalama litapunguza kwa kiasi kikubwa mateso yanayowakabili watu wa Sudan kwa kuhakikisha upitishwaji salama wa misaada ya kiutu na kufungua njia ya mchakato wa kisiasa kuelekea usitishwaji kamili wa mapigano.

Taarifa za awali aidha zimesema mjumbe maalumu wa Marekani nchini Sudan Tom Perriello atazuru mataifa kadhaa ya Afrika na Mashariki ya Kati kuanzia Machi 11 hadi 25 hii ikiwa ni kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje, iliyosema inaashiria kipaumbele cha serikali ya Marekani katika kuhakikisha inaumaliza mzozo huo wa Sudan.