1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Wahouthi wafyatua makombora kuelekea meli za Marekani

Lilian Mtono
31 Januari 2024

Wapiganaji wa Kihouthi nchini Yemen wamefyatua makombora kadhaa na kuzilenga meli za kivita za Marekani katika Bahari ya Shamu, masaa machache baada ya jeshi la Marekani kuripoti kulidungua kombora.

https://p.dw.com/p/4bssy
Meli iliyoshambuliwa na waasi wa Kihouthi katika bahari ya Sham
Meli iliyoshambuliwa na waasi wa Kihouthi katika bahari ya ShamPicha: Indian Navy/AP/dpa/picture alliance

Wanamgambo hao wanaoungwa mkono na Iran kwa miezi kadhaa wamekuwa wakifanya mashambulizi ya meli katika Bahari ya Shamu, hali iliyochochea Marekani na Uingereza kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Wahouthi hao wamefanya mashambulizi zaidi ya 30 dhidi ya meli za kibiashara, wakisema hatua hizo ni kuonyesha mshikamano na Wapalestina pamoja na kupinga vita vya Israel katika Ukanda Gaza.

Baadhi ya makampuni ya meli yamelazimika kubadili njia na kupita kusini mwa Afrika ili kuiepuka Bahari ya Shamu.

Marekani inaongoza muungano wa kulinda meli za Bahari ya Shamu na inakusudia kutumia shinikizo la kidiplomasia na kifedha kuwaorodhesha wapiganaji wa Kihouthi kama kundi la kigaidi.