1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Timu ya kampeni ya Trump yachangisha dola milioni 7.1

28 Agosti 2023

Timu ya kampeni ya aliyekuwa rais wa Marekani imesema kuwa imechangisha dola milioni 7.1 tangu kiongozi huyo wa zamani alipochukuliwa alama za vidole na picha yake ya rekodi za polisi katika gereza la Fulcon, Georgia

https://p.dw.com/p/4VdGd
Mashati ya kampeni yenye picha za Donald Trump
Mashati ya kampeni yenye picha za Donald TrumpPicha: Mario Anzuoni/REUTERS

Timu ya kampeni ya aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump imesema kuwa imechangisha dola milioni 7.1 tangu kiongozi huyo wa zamani alipochukuliwa alama za vidole na picha yake ya rekodi za polisi katika gereza la Fulcon, Georgia kwa madai ya kupanga njama ya kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Timu hiyo ya kampeni ya urais imetumia picha hiyo - ya kwanza ya kiongozi wa zamani wa Marekani - kama alama ya juhudi zake za kurudi tena Ikulu mwaka 2024.

Msemaji wa timu hiyo ya kampeni ya urais Steven Cheung ameliambia shirika la habari la AFP jana Jumapili kuwa, wamechangisha takriban dola milioni 20 katika muda wa wiki tatu, sambamba na wakati Trump alipofunguliwa mashtaka yanayohusu njama za kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Hata hivyo, shirika la habari la AFP halikuweza kuthibitisha madai hayo.

Baadhi ya wachambuzi, wameeleza kuwa picha hiyo imemuongezea Trump umaarufu mkubwa na kuilinganisha na kauli mbiu ya "Tumaini" wakati wa kampeni ya urais ya Barack Obama mnamo mwaka 2008.