1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Donald Trump kujisalimisha Alhamisi mahakamani Georgia

22 Agosti 2023

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema atajisalimisha siku ya Alhamisi kwenye mahakama iliyoko jimbo la Georgia.

https://p.dw.com/p/4VRAb
Trump atakabiliana na mashtaka ya kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.
Trump atakabiliana na mashtaka ya kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.Picha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Trump amesema siku hiyo atakamatwa na mwanasheria Mkuu wa jimbo la Georgia mwenye mrengo mkali wa kushoto, Fani Willis.

Jaji katika kesi hiyo hapo awali aliidhinisha dhamana ya dola 200,000 katika kesi ya ulaghai iliyowasilishwa dhidi ya Rais huyo wa zamani wa Marekani.

Trump na washtakiwa wengine 18 katika kesi hiyo ya kihistoria wamepewa hadi saa sita mchana siku ya Ijumaa kujisalimisha kwa mamlaka ya jimbo la Georgia.

Mbali na dhamana ya dola 200,000 kwa bilionea huyo wa chama cha Republican, Jaji wa Mahakama ya Juu ya Kaunti ya Fulton, ameweka masharti kadhaa katika makubaliano yaliyoidhinishwa kati ya waendesha mashtaka na mawakili wa Trump.