1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUhispania

Rais wa Shirikisho la Soka la Uhispania Rubiales ajiuzulu

11 Septemba 2023

Rais wa Shirikisho la Kandanda la Uhispania Luis Rubiales ametangaza hapo jana kuwa atajiuzulu.

https://p.dw.com/p/4WB4p
Luis Rubiales
Picha: Denis Balibouse/REUTERS

Amechukua uamuzi huo baada ya kuandamwa kwa wiki tatu na kashfa za kumpiga busu mdomoni mchezaji wa Uhispania Jenni Hermoso wakati timu ya taifa ya Uhispania walipoibuka washindi wa Kombe la Dunia la Wanawake.

Bildkombo Spanien Fußball | Luis Rubiales und Jennifer Hermoso
Luis Rubiales (kushoto) na Jennifer HermosoPicha: RFEF/Kim Price/Zuma/picture alliance

Shirikisho la Soka la Uhispania (RFEF) limethibitisha Jumapili usiku taarifa hiyo ya  kujiuzulu kwa Rubiales  na kubaini kuwa amejiuzulu pia katika wadhifa wake kama makamu wa rais wa shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA). Awali Rubiales alikataa kujiuzulu na kusema mchezaji huyo wa kike aliridhia kitendo hicho, madai ambayo Hermoso aliyakanusha.

Mwezi Agosti, Shirikisho la soka duniani FIFA lilimsimamisha Rubiales na hivyo hakuruhusiwa kujihusisha na shughuli zozote zinazohusiana na mpira wa miguu.