1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirikisho la kandanda Uhispania lamtaka Rubiales ajiuzulu

29 Agosti 2023

Wawakilishi wa shirikisho la soka nchini Uhispania wamemtaka mkuu wa bodi hiyo, Luis Rubiales ajiuzulu mara moja .

https://p.dw.com/p/4Vicz
Shirikisho kuu la vyama vya soka duniani,FIFA tayari limemsimamisha Rubiales.
Shirikisho kuu la vyama vya soka duniani,FIFA tayari limemsimamisha Rubiales.Picha: Gabriel Bouys/picture alliance/La Nacion/ZUMA Press

Shinikizo hilo limetokana na kitendo cha kumbusu midomoni mchezaji, Jenni Hermoso kwenye Kombe la Dunia.

Shirikisho hilo la kandanda la nchini Uhispania limechukua hatua hiyo wakati hali inazidi kutifua mzozo wa kitaifa kuhusu haki za wanawake.

Wakati huo huo kaimu mawaziri kadhaa wanamshauri Rubiales aondoke.

Hapo awali wawakilishi wengi wa shirikisho hilo walimpongeza Rubiales alipotangaza siku ya Ijumaa kuwa hatajiuzulu lakini hali imebadilika.

Jumatatu walimtaka aachie ngazi na pia wanataka mabadiliko yafanyike katika nyadhifa mbalimbali kwenye shirikisho la kandanda nchini Uhispania.

Shirikisho kuu la vyama vya soka duniani,FIFA tayari limemsimamisha Rubiales.