1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoIvory Coast

Ghana yalazimisha sare ya 2-2 na Misri

Mohammed Khelef
19 Januari 2024

Ghana imefanikiwa kulazimisha sare ya 2-2 na miamba ya soka Misri katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON inayoendelea nchini Ivory Coast.

https://p.dw.com/p/4bRaU
Michuano ya soka ya AFCON 2024 I Misri vs Ghana
Wachezaji wa Misri wakijipongeza baada ya kupata bao walipokutana na Ghana katika michuano ya AFCON Januari 18, 2024Picha: Kim Price/Newscom/picture alliance

Mohammed Kudus alifanikiwa kuyaweka kimiani magoli yote mawili ya Nyota hao Weusi.

Hata hivyo, bado matokeo hayo yanaiweka Ghana mkiani kwenye Kundi B, sambamba na Msumbiji yenye pointi moja, huku Misri ikiwa ya pili kwa pointi mbili, nyuma ya kiongozi wa kundi hilo, Cape Verde, yenye pointi 3.

Katika mechi za Kundi A, Nigeria iliwabwaga wenyeji wa michuano hiyo, Ivory Coast, kwa bao moja bila, lililowekwa wavuni kwa mkwaju wa penalti wa William Troost-Ekong katika kipindi cha pili. Ikiwa na pointi nne kibindoni, kwa sasa Nigeria imejihakikishia kuvuka awamu hii ya mtoano na kusonga mbele kwenye duru ya pili.

Kwenye mechi nyengine ya Kundi hilo la A hapo jana, Guinea ya Ikweta iliilaza Guinea-Bissau nne - mbili na kuifanya kuongoza Kundi hilo sambamba na Nigeria, zote zikiwa na pointi 4 kila mmoja.