1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yaponea chupuchupu kupoteza mchezo wa kwanza AFCON

15 Januari 2024

Timu ya soka ya Misri imeponea chupuchupu kupata fedheha kwenye mchezo wake wa kwanza wa michuano ya mataifa ya Afrika, AFCON, dhidi ya Msumbiji uliomalizika kwa sare ya bao 2-2.

https://p.dw.com/p/4bEew
Michuano ya AFCON | Misri vs. Msumbiji | Mo Salah
Mkwaju wa Penati wa Mohammed Salah ndiyo uliinusuru Misri na aibu ya kupoteza mechi mbele ya Msumbiji.Picha: Kim Price/CSM via ZUMA Press Wire/picture alliance

Mkwaju wa penati wa mshambuliaji Mohammed Salah mnamo dakika za majeruhi ndiyo uliwaokoa Misri na aibu ya kufungua pazia kwa kichapo kwenye mchezo huo wa kundi B.

Penati hiyo ilitolewa baada ya kiungo Mostafa Mohamed kuchezewa madhambi, na Salah akapachiwa wavuni mkwaju ulioinyima Msumbiji ushindi wa kwanza wa kihistoria kwenye michuano hiyo ya kandanda barani Afrika.

Kwenye mchezo mwingine wa kundi B, timu ya soka ya Ghana ilikubali idhara kwa kucharazwa hadharani bao 2-1 na vijana wa Cape Verde.

Kabla ya michezo ya kundi B, kulikuwa na mchezo wa kundi A kati ya Nigeria na Guinea ya Ikweta na ulimalizika kwa sare tasa ya bao 1-1.