1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Marekani yafanya duru mpya ya mashambulizi dhidi ya Wahouthi

23 Januari 2024

Marekani na Uingereza zimefanya duru mpya ya mashambulizi dhidi ya Wahouthi na kueleza kuwa duru hiyo ni jibu kwa mashambulizi yanayofanywa na waasi hao wa Yemen dhidi ya meli za kibiashara katika bahari ya Sham.

https://p.dw.com/p/4bZSk
Wapiganaji wa kundi la waasi wa Kihouthi
Wapiganaji wa kundi la waasi wa KihouthiPicha: Mohammed Hamoud/Anadolu/picture alliance

Mashambulizi hayo ya Marekani na Uingereza yalilenga maeneo manane ya Wahouthi nchini Yemen ikiwemo hifadhi ya silaha ya chini ya ardhi.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Marekani na Uingereza, imesema kuwa mashambulizi hayo yananuia kupunguza makali na uwezo wa Wahouthi ambao wanatishia kusambaratisha biashara ya kimataifa na kutishia pia maisha ya mabaharia wasiokuwa na hatia.

Vikosi vya nchi hizo mbili vilifanya mashambulizi ya kwanza dhidi ya Wahouthi mnamo Januari 11, na hivi karibuni Marekani iliharibu makombora 14 ya waasi hao, ambayo Washington inasema yalikuwa yamepangwa kurushwa.

Wahouthi wameapa kuendelea na mashambulizi yao na jana Jumatatu, walisema walilenga meli ya kijeshi ya Marekani ya mizigo - madai yaliyopingwa na Marekani.