1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kuijengea Somalia kambi za wanajeshi

Tatu Karema
16 Februari 2024

Marekani itajenga takribani kambi tano mpya za kijeshi kwa ajili ya jeshi la Somalia katika mradi unaolenga kuimarisha uwezo wa jeshi la nchi hiyo inayoendelea kukabiliwa na vitisho vya makundi ya itikadi kali.

https://p.dw.com/p/4cSwk
Maafisa wa usalama wa Somalia mjini Mogadishu.
Maafisa wa usalama wa Somalia mjini Mogadishu.Picha: Abukar Muhudin/AA/picture alliance

Waziri wa ulinzi wa Somalia na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani walitia saini makubaliano hayo mapema Alhamis katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. 

Makubaliano hayo yamefanyika wakati Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Nchi za Afrika nchini humo (ATMIS) kikipunguza askari wake. 

Soma zaidi: Rais mpya Somalia apongeza kurudi kwa wanajeshi wa Marekani, ahimiza maridhiano

Kambi mpya zinazopangwa kujengwa na Marekani zitahusishwa na kambi ya kijeshi ya Danab iliyoanzishwa mwaka 2017 baada ya makubaliano ya Marekani na Somalia ya kuwasajili, kuwapa mafunzo na vifaa askari 3,000 ili kuunda jeshi imara la Somalia.