1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Utawala wa sheriaUlaya

Kremlin yaionya Marekani kuingilia mambo yake ya ndani

Amina Mjahid
12 Desemba 2023

Ikulu ya Urusi imekosoa kile ilichokiita "kuingiliwa mambo yake ya ndani na Marekani" katika kesi ya kiongozi wa upinzani Alexei Navalny ambaye washirika wake wamesema hawajui aliko.

https://p.dw.com/p/4a5VW
Sheria na Haki | Mwanamke akionesha bango linaloshinikiza kuachiliwa kuachiliwa kwa iongozi wa upinzani Alexei Navalny
Mwanamke akionesha bango linaloshinikiza kuachiliwa kuachiliwa kwa iongozi wa upinzani Alexei Navalny Picha: Nikita Batalov/DW

Siku moja kabla ya tamko hilo, Marekani ilisema ina wasiwasi na taarifa kutoka kwa timu ya Navalny iliyosema haijaweza kumpata kwa wiki moja na kuripoti kuwa aliondolewa katika jela aliyokuwa akizuiliwa kwa miezi kadhaa. 

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amewaambia waandishi habari kwamba Navalny ni mfungwa aliyepatikana na hatia na anatumikia kifungo chake nchini Urusi na kuingiliwa kwa mambo ya ndani ya taifa hilo hakutakubalika. 

Soma pia:Marekani yatangaza vikwazo kwa watu na makampuni chini Urusi

Timu ya kiongozi huyo wa upinzani imesema mwanasiasa huyo anayetumikia kifungo cha miaka 19 jela amekosa kufika mahakamani kusikiliza kesi zake na kwamba mawakili wake waliambiwa aliondolewa kutoka jela alimokuwa na huenda akawa amepelekwa katika jela iliyo na adhabu kali zaidi.