1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya, Tanzania zakabiliwa na kimbunga Hidaya

Sudi Mnette
3 Mei 2024

Kenya na Tanzania zipo katika kukabiliana na kimbunga Hidaya baada ya mvua kubwa kunyesha ambayo imelivuruga eneo zima la Afrika Mashariki, na kuua zaidi ya watu 350 huku maelfu ya watu wakilazimika kuyahama makazi yao.

https://p.dw.com/p/4fSAa
Wavuvi huvua samaki mashariki mwa Kenya, Juni 22, 2023
Wavuvi huvua samaki mashariki mwa Kenya, Juni 22, 2023.Picha: Wang Guansen/Xinhua/picture alliance

Mapema ofisi ya Rais wa Kenya, William Ruto ilitangaza taadhari ya kutokea kimbunga Hidaya, ambacho kitakuwa na upepo mkali na kuathiri zaidi maeneo ya pwani, tangazo ambalo pia limetolewa kwa upande wa Tanzania ambako mvua kubwa na mafuriko vimesababisha watu 155 kupoteza maisha.

Mbali na kupoteza maisha ya watu 188 nchini Kenya tangu Machi, mafuriko hayo yamesababisha watu 165,000 kuyahama makazi yao, huku 90 wakiripotiwa kutojulikana walipo, hali ambayo serikali  imewataka raia kuwa na tahadhari.