1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yaonesha utayari wa kuzungumza na Marekani

Saleh Mwanamilongo
13 Mei 2024

Iran imeonyesha utayari wake kwa mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani. Na pia uwezekano wa nchi hiyo wa kubadili sera zake dhidi ya adui yake huyo mkubwa.

https://p.dw.com/p/4fn2K
Kamal Kharrazi
Mshauri wa sera za kigeni wa kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, Kamal Kharrazi.Picha: mehrnews

Kamal Kharazi, mshauri wa sera za kigeni wa kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amenukuliwa na shirika la habari la Iran, ISNA akisema, Wamarekani wanaelezea diplomasia kama chaguo bora zaidi, amesema Iran pia ina maoni sawa na hayo.

Kulingana na Kharazi, Iran iko tayari pia kwa mazungumzo kuhusu nishati ya nyuklia yaliyovunjika wakati wa utawala wa Donald Trump.

Hadi sasa, serikali ya kihafidhina ya Rais Ebrahim Raisi imekuwa ikikataa mawasiliano ya moja kwa moja na Marekani.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje mjini Tehran, mawasiliano ya kidiplomasia na Marekani hufanyika tu kupitia nchi rafiki kama vile Qatar na Oman na, katika baadhi ya matukio, kupitia Umoja wa Ulaya.

Hata hivyo, kauli za hivi karibuni za viongozi wa Iran zinaonesha mabadiliko ya sera za taifa hilo la kiislamu.