1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran kuwekewa vikwazo zaidi baada ya kuishambulia Israel

Amina Mjahid
18 Aprili 2024

Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa kundi la nchi tajiri kiviwanda G7, unaendelea mjini Capri Italia, ambako wanadiplomasia hao wanajadili vikwazo zaidi kwa Iran kufuatia mashambulizi yake dhidi ya Israel.

https://p.dw.com/p/4ev3o
Iran | Ebrahim Raisi
Rais wa Iran Ebrahim RaisiPicha: Iranian Presidency via ZUMA Press/picture alliance

Mashambulizi ya droni na makombora dhidi ya Israel yaliyofanywa na Iran siku ya Jumamosi ndio moja ya ajenda muhimu inayoendelea kujadiliwa katika mkutano huo. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Annalena Barbock ametoa wito kwa mataifa yote mawili yanayohasimiana kuvumiliana huku akisema muendelezo wa mashambulizi hautaifaidisha nchi yoyote.

Annalena Baerbock amesema kundi hilo linaloongozwa na Italia inayoshikilia uwenyekiti wa kupokezana, linapaswa kuchukua hatua ya pamoja dhidi ya Iran kufuatia shambulizi lake kwa Israel, akiongeza kuwa hatua za majibu ya G7 inayozijumuisha Marekani, Canada, Uingereza, Ufaransa, Japan na Umoja a Ulaya zinajadiliwa kwa kina.

Mzozo wa Mashariki ya kati wagubika mkutano wa G7 Tokyo

Huku hayo yakiendelea huko Italia, nchini Israel Waziri Mkuu wa taifa hilo Benjamin Netanyahu amesema Israel itaamua namna na vipi itakavyojibu mashambulizi ya Iran na kupuuzilia mbali wito wa washirika wake wakutaka kujizuwiya kufanya hivyo kwa hofu ya kutanua zaidi mzozo ulioko Mashariki ya kati kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.

Baada ya tamko hilo la Israel rais wa Iran Ebrahim Raisi amekuwa akionya mara kwa mara kuwa uvamizi wowote dhidi yake utajibiwa vikali. Iran iliishambulia Israel baada ya tuhuma kwamba Israel ilifanya shambulizi katika ubalozi wake mdogo nchini Syria na kusababisha mauaji ya makamanda wake 7.

China na Inonesia zakataka makubaliano ya kusitisha mapogano Gaza kufikiwa haraka

Indonesien -Retno Marsudi
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Indonesia Retno Marsudi Picha: picture-alliance/dpa/A. Weda

Kwengineko Israel bado inaendelea na vita vyake dhidi ya wanamgambo wa Hamas na imeendelea kushambulia baadhi ya maneno ya ukanda wa Gaza. China na Indonesia kupitia mawaziri wake wa mambo ya nchi za nje wametoa wito wa makubaliano ya haraka ya kusitisha mapigano katika ukanda huo baada ya kukutana mjini Jakarta.

Retno Marsudi wa Indonesia na mwenzake Wang Yi  wa China wamesikitishwa pia na hali ya kibinaadamu inayoendelea kuwa mbaya mjini Gaza. Marsudi amwaambia waandishi habari kwamba wanaunga mkono suluhu ya kuwa na mataifa mawili ili kumaliza kabisa mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miezi sita sasa.

"Tuna maoni sawa juu ya umuhimu wa wanaohasiamiana kuvumiliana na umuhimu wa kuzuwia mgogoro kutanuka zaidi. Naamini pia China itatumia nguvu yake kuzuwia hilo kufanyika, na tuna maoni sawa juu ya umuhimu wa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza na suluhu ya mataifa mawili," alisema Retno Marsudi.

Netanyahu asema Israel itajiamulia yenyewe masuala yake ya usalama

Hapo kesho Ijumaa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa unatarajiwa kulipigia kura ombi la Palestina la kutaka kutambuliwa kama nchi mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa, hatua ambayo mshirika mkubwa wa Israel, Marekani inatazamiwa kupinga. Kwa azimio hilo kupita kutahitajika uungaji mkono wa nchi tisa kati ya 15 zilizoko katika Baraza hilo, na bila ya kuwa na kura ya turufu kutoka Marekani, Uingereza, Ufaransa, urusi au China. Wanadiplomasia wanasema huenda azimio hilo likaungwa mkono na nchi 13 na hiyo huenda ikaifanya Marekani kutumia kura yake hiyo ya turufu kupinga azimio hilo.

Baerbock ziarani Israel tena kusaka suluhisho la mgogoro

afp/reuters/ap