1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hichilema bado ana matumaini kupatikana wachimba madini 25

Bruce Amani
6 Desemba 2023

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amesema bado ana matumaini kuwa takribani wachimba madini 25 wasio rasmi walionasa mgodini siku nne zilizopita bado wako hai.

https://p.dw.com/p/4ZpX4
Rais Hakainde Hichilema wa Zambia.
Rais Hakainde Hichilema wa Zambia.Picha: picture alliance/dpa/AP

Wachimbaji hao wamekwama baada ya kutokea kwa maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Mvua hizo ziliyafanya machimbo hayo kufurika katika maeneo manne tofauti ya migodi ya shaba. 

Soma zaidi: Yellen azuru Zambia kujadilia madeni ya China, afya ya umma

Kulingana na serikali ya Zambia machimbo hayo ni ya mgodi wa Seseli yaliyo katika eneo la Chingola umbali wa kilomita 250 kaskazini mashariki mwa Lusaka.

Juhudi za uokoaji zinaendelea wakati timu za uokoaji wakiwemo wanajeshi na makampuni mengine makubwa yakichukua tahadhari kutokana na utelezi unaopunguza kasi ya operesheni hiyo