1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoIvory Coast

Emerse Fae: Safari ya ushindi wa Ivory Coast ni kama miujiza

12 Februari 2024

Mshambuliaji Sebastian Haller amekuwa shujaa wa timu ya taifa ya Ivory Coast baada ya kufunga bao la ushindi katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON dhidi ya Nigeria.

https://p.dw.com/p/4cJvY
Kombe la Mataifa ya Africa AFCON |  Fae Emerse
Kocha wa muda wa Ivory Coast Fae EmersePicha: Sydney Mahlangu/Sports Inc/empics/picture alliance

Baada ya kuponea kutolewa kutoka hatua ya makundi, ikiwa ni pamoja na kufutwa kazi kwa kocha Jean Louis Gasset, Ivory Coast imeweka historia kwa kushinda taji lao la tatu la AFCON baada ya kuibuka kidedea mwaka 1992 na 2015.

Kocha wa muda Emerse Fae amesema, "Kwa kweli, ni zaidi ya hadithi bado siamini kwamba tumeshinda. Ninapofikiria tulichopitia wakati michuano inaendelea, zile nyakati ngumu, tukitoka nyuma na kupata ushindi katika dakika za mwisho mwisho, ni kama miujiza. Tumeshinda kwa sababu hatukukata tamaa, tulipambana hadi mwisho, tulionyesha sisi ni wanaume, tunajinyanyua baada ya kuanguka."

Soma pia: Nigeria yawataka raia wake Afrika Kusini kuwa na hadhari

Kocha wa Super Eagles Nigeria Jose Peseiro ameipongeza Ivory Coast na kukiri kwamba vijana wake walizidiwa maarifa uwanjani.

"Timu yetu imefanya vizuri katika michuano hii, lakini leo Ivory Coast walikuwa bora, walikuwa na mchezo mzuri sana. Timu yetu haikucheza vizuri au hata kuonyesha kiwango cha juu. Ni kweli, sio kiwango tulichokitarajia. Hili linapotokea, kitu pekee ninachoweza kusema ni kuipongeza Ivory Coast, walikuwa bora kuliko sisi," ameeleza Peseiro.