1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump apania kumuangusha Haley South Carolina

Lilian Mtono
24 Februari 2024

Donald Trump na Nikki Haley watachuana Jumamosi hii katika kura ya mchujo ya jimbo la South Carolina ya kumtafuta mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican.

https://p.dw.com/p/4cq48
Marekani, Washingtorn | Donald Trump na Nikki Haley
Donald Trump wakati huo akiwa rais wa Marekani akiwa na Nikki Haley aliyekuwa balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Oktoba 9, 2018. Hivi sasa ni maadui wakubwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kugombea urais Picha: Jonathan Ernst/REUTERS

Trump, aliyeiongoza Marekani kwa muhula mmoja, anatazamiwa kumshinda Haley aliyewahi kuliongoza jimbo la South Carolina akiwa Gavana kwa mihula miwili. 

Haley alikuwa maarufu kwenye jimbo hilo kwa miaka sita kabla ya kuteuliwa na Trump kuwa balozi kwenye Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2017, lakini kwa sasa Trump anaungwa mkono na vigogo wa chama na karibu theluthi mbili ya wapiga kura kwenye uchunguzi wa maoni. Trump tayari alikwishashinda kura za mchujo zilizotangulia kwenye majimbo ya Iowa na New Hampshire.

Baadhi ya wapiga kura waliojitokeza katika mji mkuu wa jimbo hilo wa Columbus siku ya Alhamisi, waliliambia shirika la habari la AFP kwamba wanaridhishwa na wagombea ingawa mmoja wao alisema anadhani Haley hakuwa tayari kushika wadhifa huo wa juu kabisa na mwingine akimkosoa Trump kwa kuleta migawanyiko.