1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Beijing yapeleka zana za kijeshi karibu na Taiwan

Lilian Mtono
27 Januari 2024

Beijing imepeleka ndege 33 za kivita na manowari sita za kijeshi karibu na kisiwa cha Taiwan, hii ikiwa ni kulingana na Waziri wa Ulinzi wa Taiwan amesema Jumapili.

https://p.dw.com/p/4bkYB
Ujia wa Taiwan | China inazidi kuiongezea shinikizo Taiwan
Meli za kivita za China zilipogunduliwa na Marekani zikivuka uji wa bahari wa Taiwan, Juni 3, 2023Picha: Global News/REUTERS

Kulingana na waziri huyo, Taiwan pia iliijibu hatua hiyo kwa kupeleka vikosi vyake.

Idadi ya kila siku ya ndege za kivita zinazorushwa na China karibu na anga ya Taiwan imevunja rekodi tangu Taiwan ilipofanya uchaguzi wa kidemokrasia wa rais na wabunge, Januari 13.

Hatua ya Beijing ya kuongeza shinikizo la kijeshi dhidi ya Taiwan inafuatia ziara ya siku ya tatu ya wabunge wa Marekani iliyomalizika jana Ijumaa, ukiwa ni ujumbe wa kwanza rasmi wa Marekani tangu alipochaguliwa rais William Lai Ching-te.

Ndege 13 kati ya 33 za kijeshi za China zilivuka mstari usio rasmi kwenye Ujia wa Taiwan, unaokigawa kisiwa hicho na China, imesema wizara hiyo.