1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden asema mahusiano na China yanafuata "mkondo sahihi"

20 Juni 2023

Rais Joe Biden wa Marekani amesema anaamini mahusiano kati ya nchi yake na China yanachukua mwelekeo mzuri na ameashiria kwamba kuna mafanikio fulani.

https://p.dw.com/p/4Snj2
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akutana na Xi Jinping
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akutana na Xi JinpingPicha: Li Xueren/Xinhua/IMAGO

Rais Biden ametoa matamshi hayo  alipokuwa akijibu maswali ya waandishi habari waliotaka mtazamo wake juu yakilichopatikana baada ya kukamilika kwa ziara ya Blinken nchini China.

Kiongozi hiyo amesema Blinken amefanya kazi kubwa iliyowezesha kufikiwa makubaliano ya kusawazisha uhasama baina ya Washington na Beijing kwa dhima ya kuzuia hali hiyo kutegeuka kuwa mzozo.

Mwadiplomasia hiyo wa Marekani alihitimisha ziara yake hapo jana baada ya kukutana na viongozi wa ngazi ya juu wa China ikiwemo rais Xi Jinping.

Alikuwa mjini Beijing kusisitiza umuhimu wa China na Marekani kuwa na mahusiano mazuri na kuepuka mivutano.