1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Balozi wa zamani wa Marekani na jasusi wa Cuba afungwa jela

Sylvia Mwehozi
13 Aprili 2024

Balozi wa zamani wa Marekani Victor Manuel Rocha ambaye alikiri kufanya ujasusi kwa ajili ya Cuba, amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.

https://p.dw.com/p/4eiQ9
Bendera-Cuba-Marekani
Bendera ya Marekani na CubaPicha: Joe Raedle/Getty Images

Balozi wa zamani wa Marekani Victor Manuel Rocha ambaye alikiri kufanya ujasusi kwa ajili ya Cuba, amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela. Mbali na adhabu hiyo, atatakiwa kulipa faini ya Dola 500,000 na kufichua taarifa za kijasusi alizoshirikiana na Cuba.

Rocha, mwenye umri wa miaka 73, alikamatwa mwezi Disemba kwa kile maafisa wa Marekani walichokitaja kuwa ni mojawapo ya ujasusi wa kiwango cha juu na uliofanyika kwa muda mrefu.

Soma: Cuba na Marekani: Marafiki walio na nyuso mbili

Mwanadiplomasia huyo wa zamani aliunga mkono kwa siri harakati za chama tawala cha kikomonisti cha Cuba na kufanya ujasusi dhidi ya Washington kwa zaidi ya miongo minne.

Aliwahi kuhudumu kama balozi wa Marekani nchini Bolivia kuanzia mwaka 2000 hadi 2002 na kufanya kazi kwa kipindi cha miaka 20 katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani.