1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ardhi inayodaiwa kumilikiwa na Ruto yaibua mzozo

Wakio Mbogho13 Machi 2024

Mzozo wa ardhi ya Ndabibi katika kaunti ya Nakuru unaendelea kugonga vichwa vya habari ambapo bunge la kitaifa sasa limeelezwa kwamba zaidi ya watu 140,000 wamefurushwa kutoka kwenye makao yao.

https://p.dw.com/p/4dSnV
Mlima Kenya
Sehemu ya msitu karibu na mlima KenyaPicha: Ed Ram/Getty Images

Akizungumza kwenye bunge la Seneti, seneta wa Naivasha Tabitha Keroche, amewasilisha ombi la kutaka uchunguzi na ufafanuzi kuhusu kufurushwa kwa watu laki moja, na elfu arobaini kutoka kwenye shamba la Ndabibi lililoko Naivasha.

Mizozo ya ardhi: Kenya yatakiwa kushughulikia sakata la ardhi

"Tunataka kujua sababu ya kuharibiwa kwa makaazi elfu 40,000, kafyu zisizohalali, wizi wa mazao ya mashamba unaofanywa na polisi, wakaazi kufyatuliwa risasi wakiwa nyumbani kwao, vurugu, ubakaji na watu zaidi ya mia moja kukamatwa na kuzuiliwa kinyume na sheria.”

 William Ruto
Rais wa Kenya William RutoPicha: Monicah Mwangi/REUTERS

Wiki iliyopita watu 19 walikamatwa na kufikishwa mahakamani katika kaunti ya Nakuru baada ya kuvunja ua kwenye shamba hilo la Ndadidi lenye ukubwa wa eka elfu tano, na kuharibu mali ya mamilioni ya pesa. Wakaazi hao ambao wengi wao ni wakulima wanadai ardhi hiyo ni yao, wengi wao wakiwa wameishi hapo kwa miaka mingi.

 "Tunauliza kwani sisi hatuna haki, kuna mama ameshikwa sahizi tunavyoongea, ana Watoto, ni siku tano sasa. Tunauliza ni kwanini hawapelekwi kotini? Na sisi tumeumizwa hata mwenzetu ameumizwa mguu, " alisema David Chege.

Mkaazi mwingine Joshua Manasi naye aliuliza "Mimi ni mmoja wa wale waliopewa hili shamba, nilikuja hapa mwaka 1957. Haya shule imechukuliwa, hospitali imechukuliwa, hata sisi tunashindwa tutatokea wapi?”

Soma: Rais Uhuru aanza kutatua tatizo la ardhi Kenya

Wametishia kufunga shule eneo hilo iwapo mzozo huo hautatatuliwa na wapewe hati miliki ya ardhi. Hata hivyo kwenye baraza la umma lililoandaliwa na viongozi wa eneo hilo, naibu kamishna wa Nakuru Mutua Kisilu amesema hawatasita kuimarisha usalama eneo hilo.

Mbiu ya Mnyonge: Ardhi ya kijamii

"Wiki hii najua tumekimbizana sana na sio kupenda kwetu, lakini sasa hauwezi kuweka kidole kwa Rais wangu halafu ninyamaze. Watu walisema ati watafunga shule na kuna watu kweli wanajua kuongea mambo hawawezi kweli, unafunga shule ya nani kweli?”

Fuatilia habari hii: Kenya: Wazee wa wamijikenda waandamana

Mbunge wa Naivasha Jayne Kihara amemtambulisha Rais William Ruto kama mmiliki halali wa ardhi hiyo ya Nadabibi. Anasema Rais alinunua ardhi hiyo kihalali kutoka kwa Benjamin Kulei aliyekuwa mwanadiplomasia katika utawala wa Rais mstaafu marehemu Daniel Moi.

"Nimekuja hapa ndio kama kuna shamba ya mtu hapa ambayo Rais amechukua, aje hapa nimpeleke kwa Rais, ndio amuambie mheshimiwa Rais ulichukua shamba langu.”

Hata hivyo, Seneta Tabitha Keroche amelieleza bunge kuwa mwezi Februari mwaka huu mahakama ya Naivasha.