1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajasirimali wa kiafrika – Wenye mafanikio na wenye kuwajibika

10 Mei 2012

Hulala kidogo sana, hawafahamu neno „starehe“ lakini wanaipenda kazi yao na wanajitoa kwa jamii wanamoishi. Hili ni jambo linalowaunganisha wafanyabiashara wote wa Kiafrika tunaowatambulisha katika mfululizo wetu mpya.

https://p.dw.com/p/14sSA
Learning by Ear – African entrepreneurs Fotograf | Bildagentur: © RICCARDO GANGALE RICCARDO GANGALE / The New York T / Redux / LAIF (Business man, Computer) ACHTUNG!! DIE DEUTSCHE WELLE HAT DIE NUTZUNGSRECHTE NUR BIS 1.9.2013!! EINSTELLUNGSDATUM: 09.09.2011
Picha: LAIF

Katika mfululizo huu tunawatambulisha wajasiriamali kutoka Afrika waliobobea katika kazi yao na ambao baada ya safari ndefu hatimaye wamekuwa wafanyabiashara wenye mafanikio. Tutamtembelea mtengenezaji wa michezo ya watoto kutoka Afrika Kusini, mtu aliyeleta mageuzi ya vyoo nchini Kenya, mfanyabiashara mkubwa katika sekta ya mawasiliano kutoka Sudan anayeishi London, Uingereza na wengine wengi. Hawajafanikiwa katika kazi zao tu bali pia wanarudisha sehemu ya mafanikio yao katika jamii kwa namna moja au nyingine.

Wajasiriamali wetu wanazungumza wazi juu ya changamoto walizokumbana nazo katika kuelekea kwenye tabaka la juu la jamii, vikwazo vilivyowakumba na kile kilichowapa moyo. Kupitia simulizi zao pamoja na uzoefu wao, wasikilizaji watafahamu jinsi ya kujiajiri wenyewe pamoja na nafasi abazo ajira hiyo inaleta kwa mtu binafsi na hata kwa ukuaji wa uchumi wa taifa.

Vipindi vya Deutsche Welle “Learning by Ear – Noa Bongo! Jenga Maisha Yako” vinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharic.