1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushiriki wa Kisiasa - Jinsi ya kujihusisha

29 Aprili 2011

Siasa haihusiani tu na bunge na serikali. Ushiriki katika siasa huanzia nyumbani! Hata kubadilisha kitu katika eneo mtu analoishi kunaweza kuleta mageuzi makubwa.

https://p.dw.com/p/NTor
Ushiriki wa kisiasa unavuka mipaka ya kupiga kura kwenye chaguziPicha: gettyimages

Kupitia vipindi vyake kuhusu masuala ya familia - jinsi ya kuwa mshiriki katika kisiasa mradi wa Learning by Ear - Noa Bongo Jenga Maisha Yako unawaeleza wasikilizaji wake kuhusu maisha ya kila siku ya familia ya kiafrika na kuonyesha jinsi maamuzi ya kisiasa yanavyopitishwa hata katika maisha ya kila siku. V

ipindi hivi vinafuatilia maisha ya ndugu watatu wanaofuatilia kutimiza ndoto zao bianfsi. Betty, aliye wa mwisho, ni muimbaji mwenye kipaji anayetaka kuunda kwanya shuleni. Ronnie ana ari ya kuwa mchezaji kandanda na anataka kuwa kapteni wa timu yake. Eveline, ambaye ndiye mkubwa wao, amemaliza tu masomo yake ya shule ya sekondari na angependa kuwa diwani.

Kuelewa mchakato wa kijamii na kisiasa

Katika jitihada zao, ndugu hawa watatu wanalazimika kukabiliana na vikwazo mbalimbali. Matatizo haya yanahusiana na kanuni maalum na kijamii na kisiasa kama vile uongozi, ufisadi, kujenga miungano, kuripoti habari na vyama vya kisiasa. Sio mipango yote ya vijana hawa chipukizi ambayo inafaulu, lakini Betty, Ronnie na Eveline wanajifunza kutokana na makosa yao wenyewe. Juu ya yote hayo, washirika wachanga kisiasa wanaanza kuelewa mambo mengi kuhusu maana ya ushiriki wa kisiasa katika maisha halisi.

Vipindi vya “Learning by Ear” ‘ Noa bongo Jenga Maisha yako’ vinasikika katika lugha sita; Kingereza, Kifaransa, Kiswahili, Kihausa, Kireno na Amharic. Na kufadhiliwa na wizara ya nchi za kigeni ya Ujerumani