1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maajabu ya kila siku - Elimu ya jumla

1 Septemba 2008

Dunia yetu imejaa mambo kadhaa ya ajabu ambayo hata hatuyafikirii. Watu wachache wanajua ujumbe mfupi yanakopita kutoka simu moja ya mkononi hadi nyingine na wachache zaidi wanajua kwa nini matairi ya gari ni meusi?

https://p.dw.com/p/DnKf
Picha: V8 Verlag, Sebastian Pfuetze

„Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinawachukua wasikilizaji wake katika safari ya maisha ya kila siku. Vipindi hivi vinachunguza mambo mbali mbali ya ajabu ambayo si lazima kwamba yanajadiliwa shuleni. Kwa mfano, maripota wetu wanaelezea jinsi mifuko ya plastiki inavyotengenezwa na kwa nini inaweza kuwa na athari katika mazingira.

Mambo muhimu na uasili

Vipindi vyetu vinaangalia pia watu wanaofanya mapenzi na wanyama wanaotuzunguka. Tunaangalia masuala ya uasili kama kwa nini viazi mbatata vinalainika wakati vikichemshwa wakati mayai yanakuwa magumu. Kuna aina nyingi ya elimu inayowazunguka wasikilizaji wake. Kwa vipindi vya „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ wasikilizaji wake watakuwa na nafasi ya kufahamu yote hayo.

„Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharik. Kwa taarifa zaidi ama kusikiliza vipindi, tafadhali tembelea tovuti yetu: www.dw-world.de/lbe „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinadhaminiwa na wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani.