1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu zashuka uwanjani katika Champions League

Admin.WagnerD30 Septemba 2014

Paris St.German ya Ufaransa inakabana koo na Barcelona ya Uhispania leo Jumanne katika mpambano ambao unatarajiwa kuwa wa vuta nikuvute wa Champions League katika uwanja wa Parc des Princes.

https://p.dw.com/p/1DNVy
Paris Saint-Germain
Picha: AFP/Getty Images

Barca iliitoa Paris St German miaka miwili iliyopita kwa sheria ya goli la ugenini katika robo fainali na hali inaelekea kujirudia yenyewe, ambapo makocha Laurent Blanc na Luis Enrique walikuwa wachezaji wa Barca kuanzia mwaka 1996-97, na mshambuliaji wa PSG Zlatan Ibrahimovic bado ana donge na klabu hiyo baada ya kufurushwa mwaka 2010 baada ya msimu mmoja tu.

Ibrahimovic anauguza maumivu ya kifundo cha mguu lakini anataka sana kuwa fit wakati wa pambano hilo la kundi F.

Bayern Munich itakuwa mjini Moscow ikipimana nguvu na CSKA Moscow katika uwanja wa Khimki lakini uwanja huo kesho hautakuwa na watazamaji kutokana na shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA kuamua kuiadhibu CSKA kucheza mchezo mmoja bila mashabiki wake kutokana na tabia ya kibaguzi ya mashabiki wake wakati ikipambana na mashabiki wanaoonesha tabia ya kibaguzi barani Ulaya.

Fußball Bundesliga 5. Spieltag FC Bayern München SC Paderborn
Vijana wa Pep Guardiola wanapigiwa upatu kufika fainaliPicha: Reuters/Michael Dalder

Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amekasirishwa kwamba adhabu hiyo dhidi ya CSKA ina maana kwamba mashabiki wa timu hiyo pia hawawezi kwenda mjini Moscow kuipa nguvu timu yao.

Katika michezo mingine kesho mabingwa Real Madrid wanapambana na Ludogorets ya Bulgaria katika mchezo wa kundi B. Basel inakwaana na Liverpool ya Uingereza, wakati Atletico Madrid inataka kurejea katika dimba hilo baada ya kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Olympiacos Piraus kwa kuikaribisha Juventus Turin ya Italia , ambayo ilianza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malmo katika kundi A.

Siku ya Jumatano viongozi wa ligi ya Uingereza Chelsea iko nyumbani kwa Sporting Lisbon baada ya kupata sare katika mchezo wa kundi G dhidi ya Schalke 04. Arsenal inaikaribisha Galatasaray ya Uturuki katika kundi D ambapo Borussia Dortmund ina lenga kumuondoa mdudu mbaya anayewafuata katika ligi ya Ujerumani Bundesliga kwa kupata ushindi dhidi ya Anderlecht ya Ubelgiji kufuatia ushindi mnono katika mchezo wa kwanza dhidi ya Arsenal.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / dpae / rtre , ZR
Mhariri: Iddi Ssessanga