1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky asema hayuko tayari kuzungumza na Urusi

Josephat Charo
6 Novemba 2023

Rais Volodymyr Zelensky wa Urusi amesema hayuko tayari kufanya mazungumzo na Urusi mpaka iwaondoe wanajeshi wake walioivamia Ukraine.

https://p.dw.com/p/4YR1B
Ukraine | Krieg | Präsident Wolodymyr Selenskyj
Picha: Presidential Office of Ukraine/SvenSimon/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hayuko tayari kuzungumza na Urusi mpaka wanajeshi wake walioivamia Ukraine watakapoondoka, huku serikali ya mjini Kyiv ikichunguza shambulizi lililofanywa dhidi ya wanajeshi wake.

Maafisa kutoka Marekani na Ulaya, wanaripotiwa kupendekeza yafanyike mashauriano kufikisha mwisho mzozo wa miezi 20, taarifa ambayo rais Zelensky aliikanusha jana Jumapili.

Zelensky amekiambia kituo cha televisheni cha NBC kwamba Marekani inafahamu hayuko tayari kuzungumza na magaidi kwa sababu kauli yao haina maana. Ametaka wanajeshi wa Urusi waondoke kutoka himaya ya Ukraine kabla ulimwengu kugeukia diplomasia. Zelensky amekiri vita vimefikia hali ngumu na akasisitiza juu ya umuhimu wa mifumo zaidi ya ulinzi wa anga kufikisha mwisho udhibiti wa Urusi wa anga.

(afpe)