1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky atoa mwito wa umoja kwa nchi za NATO

Zainab Aziz
9 Oktoba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy leo Jumatatu ameliambia Bunge la Jumuiya ya Kujihami ya NATO mjini Copenhagen, nchini Denmark, kwamba sasa sio wakati wa kujiondoa kwenye maswala ya kimataifa.

https://p.dw.com/p/4XHv7
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa na Katibu Mkuu wa NATO Jens StoltenbergPicha: Sergei Supinsky/AFP/Getty Images

 Zelensky amesisitiza juu yaumoja wa nchi za Magharibikatika kukabiliana na matukio ya kimataifa.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen ameliambia bunge hilo la NATO kwamba nchi yake inashughulikia kuupanua na kuuimarisha muungano wa nchi zilizojitolea kuipa Ukraine ndege za kivita aina ya F-16.