1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya Wajerumani milioni 4 walitafuta ajira mwaka 2019.

Amina Mjahid
9 Oktoba 2020

Takwimu zaonesha watu milioni 4.4 Ujerumani walitafuta ajira au za ziada mwaka 2019. Idadi hiyo ni ndogo kuliko mwaka 2018 lakini kuna hofu huenda ukosefu wa ajira ukaongezeka mwaka 2020 kutokana na janga la corona.

https://p.dw.com/p/3jhO8
Deutschland Frankfurt a.M. | Lufthansa-Hauptversammlung | Protest Mitarbeiter
Picha: Reuters/K. Pfaffenbach

Kulingana na utafiti uliyochapishwa siku ya Ijumaa (10.09.2020) zaidi ya Wajerumani milioni 4 aidha walitafuta kazi au kutaka kufanya kazi zaidi mwaka 2019.


Kiwango hiki kilishuka kwa asilimia 4 kulingana na takwimu za mwaka 2018, na huu ndio umekuwa mwenendo wa karibia kila mwaka ndani ya muongo mmoja uliopita. Kwa sasa haijabainika wazi iwapo janga la virusi vya corona mwaka 2020 uliosababisha wengi kukosa ajira litasababisha watu zaidi kukosa ajira hizo.


Idadi hiyo iliyotolewa na afisi ya ujerumani inayoshughulikia masuala ya takwimu ilionyesha kuwa watu milioni 1.4 walio kati ya miaka 15 hadi 74 wako mbioni kutafuta ajira. Na asilimia 2.1 wangelipenda kufanya kazi masaa mengi kila wiki, huku watu wengine 900,000 wakitafuta kazi lakini sio ya haraka bali katika siku za usoni.

Soma pia: Vyama tawala Ujerumani vyapambana na mageuzi ya ajira, uhamiaji

Lakini takwimu hizo pia zimeonyesha kuna watu milioni 1.5 nchini Ujerumani ambao wangelipenda kufanya kazi masaa machache. Idadi hii imekuwa na kufikia elfu 47,000 kutoka mwaka 2018 hadi 2019.

Idadi hiyo hata hivyo haikujumuisha idadi ya watu ambao hawafanyi kazi na kutotafuta kazi ambako kuna watu milioni 1.2 walioingia katika kundi hili nchini humo mwaka 2019.

Mfumo wa Ujerumani wa kufanya kazi wa "kazi ya muda mfupi" ilipelekea watu kubakiza kazi zao lakini kupunguza masaa ya kazi kufuatia janga la corona huenda limesababisha kutopungua sana kwa ukosefu wa kazi mwa 2020.

Hilo limefnya kampuni kadhaa zikakosa kuwa na biashara ya kawaida hatua inayoashiria kuwa mwaka 2020 huenda huenda idadi ya wanaotafuta kazi ikaongezeka.

Kuna hofu huenda ukosefu wa ajira ukaongezeka Ujerumani kufuatia janga la corona
Kuna hofu huenda ukosefu wa ajira ukaongezeka Ujerumani kufuatia janga la coronaPicha: Michael Dalder/Reuters