1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WFP yafikisha msaada wa chakula Darfur

6 Aprili 2024

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limefikisha msaada unaohitajika katika eneo lililoharibiwa na vita la Darfur nchini Sudan na kuonya kuwa hali ya njaa inaweza kuwa mbaya zaidi.

https://p.dw.com/p/4eTjx
Chakula cha msaada
Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) linasema limefikisha sehemu ya msaada unaohitajika kwa watu wa Darfur, magharibi mwa Sudan.Picha: EBRAHIM HAMID/AFP/Getty Images

Kulingana na Umoja wa Mataifa takribani watu milioni 25, ambao ni zaidi ya nusu ya idadi ya watu wa Sudan, wanahitaji msaada wa haraka, ikiwa ni pamoja na karibu milioni 18 ambao wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula. 

Soma zaidi: WFP: Machafuko ya Sudan yanaweza kusababisha mgogoro wa kikanda

Msemaji wa WFP nchini humo, Leni Kinzli, alisema misafara miwili ya misaada ilivuuka katika eneo la magharibi kutoka nchi jirani ya Chad ikiwa imebeba msaada wa chakula na lishe kwa watu wapatao 250,000 wanaokabiliwa na njaa kali.

Msemaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Margaret Harris, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mahitaji ya kibinaadamu nchini Sudan ni makubwa sana.