1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Haiti: Ghasia za magenge nchini ''ni sawa na eneo la vita''

Tatu Karema
26 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Haiti Jean Victor Geneus, ameomba kutumwa kwa kikosi cha kimataifa katika nchi hiyo inayokabiliwa na mzozo na kuliambia Baraza la Usalama la UN kwamba ghasia za magenge nchini humo ni za kinyama

https://p.dw.com/p/4bgrP
Mwandamanaji ajibizana na polisi wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya maafisa wa polisi nchini Haiti yaliofanywa na magenge ya wahalifu mjini Port -au-Prince mnamo Januari 26,2023
Maandamano ya kupinga mauaji ya maafisa wa polisi nchini HaitiPicha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Geneus ameliambia baraza hilo kwamba haijapita miaka miwili ambapo anakuja tena mbele ya baraza hilo kuchora picha ambayo ni ya kusikitisha zaidi na ambayo ni ya giza kila wakati ya hali ya usalama na kibinadamu nchini Haiti.

Watu wa Haiti wamechoka

Genus ameongeza kuwa watu wa nchi hiyo hawawezi kuvumilia zaidi na anatumaini kwamba hii ni mara ya mwisho atakayozungumza kabla ya kupelekwa kwa kikosi hicho cha kimataifa kuwasaidia maafisa wa usalama nchini humo.

Hakuna tofauti kati ya ukatili nchini Haiti na ukatili wa vita na mizozo ya silaha 

Geneus amesema ikiwa Haiti itachapisha takwimu za kila siku kuhusu kile alichosema ni ukatili unaofanywa dhidi ya Wahaiti na magenge yenye silaha, watu wataelewa kwamba hakuna tofauti kati ya ukatili wanaovumilia na vitisho na ukatili wa vita na mizozo ya silaha mahali pengine, ambayo imevutia hisia za dunia.

Waakilishi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wapigia kura rasimu ya azimio katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York mnamo Desemba 29, 2023
Baraza la Usalama la Umoja wa MataifaPicha: Eskinder Debebe/UN Photo/picture alliance/Xinhua News Agency

Kenya yapiga hatua katika maandalizi ya kupeleka kikosi chake Haiti

Balozi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa Martin Kimani, amesema serikali yake inapiga hatua muhimu katika maandalizi ya kupeleka maafisa wake katika misheni hiyo.

Soma pia:Viongozi wa makundi ya uhalifu Haiti wawekewa vikwazo

Haiti imeshuhudia ukosefu wa usalama kwa miaka mingi, uliochangiwa na mauaji ya rais Jovenel Moise mwaka wa 2021.

Soma pia:Haiti kujadili na Kenya juu ya kupelekwa askari

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa siku ya Jumanne, imesema kuwa magenge sasa yamekithiri katika maeneo mengi nchini humo na mauajiyameongezeka kwa zaidi ya mara mbili mwaka jana kufikia takriban 4,800.