1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 6 wafa baada ya boti 2 kuzama katika Ziwa Victoria

Zainab Aziz
2 Januari 2024

Polisi nchini Uganda imethibitisha vifo vya watu sita kufuatia mikasa miwili kwenye Ziwa Victoria ambapo boti mbili zilizama usiku wa kuamkia Jumanne.

https://p.dw.com/p/4ao8C
Wavuvi wa Uganda
Wavuvi katika Ziwa Victoria nchini UgandaPicha: AP

Polisi nchini Uganda imethibitisha vifo vya watu sita kufuatia mikasa miwili kwenye Ziwa Victoria ambapo boti mbili zilizama usiku wa kuamkia wa leo, Jumanne.

Kulingana na taarifa za awali, vyanzo vya ajali hizo ni hali mbaya ya hewa pamoja boti hizo kubeba mizigo uliopindukia uwezo wao, zikiwemo shehena za mkaa na samaki.Wavuvi ziwa Victoria waomba leseni za A.Mashariki 

Makundi ya wavuvi yanaendelea kutafuta miili ya watu wengine ambao wanadhaniwa walikuwa abiria kwenye boti hizo zilizokuwa zinasafirsha bidhaa kutoka visiwani kuelelekea fukwe jirani na mji wa Masaka kusini mwa Uganda.

Angalau watu watano walionusurika katika mikasa hiyo wamesaidiwa na wavuvi na wanavijiji. Matukio ya watu kufa maji hutokea kwenye ziwa hilo hasa katika vipindi wa hali mbaya ya hewa, huku wasafiri wengi wakipuuza matumizi ya vifaa vya usalama kwenye vyombo.