1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMsumbiji

Watu 11 wafariki kutokana na kimbunga nchini Malawi

John Juma
13 Machi 2023

Watu wapatao 11 wamekufa katika mji wa Blantyre, Malawi na wengine 16 hawajulikani walipo baada ya kimbunga Freddy kuikumba nchi hiyo mwishoni mwa juma.

https://p.dw.com/p/4Ob63
Mosambik | Zerstörung durch Zyklon Freddy
Picha: ALFREDO ZUNIGA/UNICEF /AFP

Msemaji wa polisi ya Malawi, Peter Kalaya ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba timu ya uokozi inawatafuta watu katika vitongoji vya Chilobwe na Ndirande, ambavyo vimeathiriwa vibaya.

Kwa mujibu wa Kalaya, inahofiwa kuwa baadhi ya watu ambao hawajulikani walipo wamefunikwa na kifusi na timu yao inashirikiana na mashirika mengine ya kitaifa.

Kimbunga Freddy kimevunja rekodi za muda na nguvu ya vimbunga vya kitropiki katika eneo la pwani ya kusini mwa Afrika.

Kimelikumba eneo la katikati ya Msumbiji, siku ya Jumapili, kabla ya kuelekea Malawi usiku kucha na kusababisha mvua kubwa na upepo mkali.