1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNiger

Wanajeshi 10 wauawa Niger na wanaoshukiwa kuwa magaidi

12 Februari 2023

Wanajeshi 10 wameuawa na wengine 13 wamejeruhiwa katika shambulizi la kuvizia linaloshukiwa kuendeshwa na kundi la "magaidi wenye silaha" kusini magharibi mwa Niger katika eneo la Banibangou, karibu na mpaka wa Mali.

https://p.dw.com/p/4NNrX
Nigrische Spezialkräfte, die von der Bundeswehr ausgebildet werden Nigeria
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Hayo yameelezwa leo na wizara ya ulinzi ya Niger iliyosisitiza kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka kutokana na shambulizi la siku ya Ijumaa, kwani watu wengine 16 bado haijulikani walipo.

Taarifa hiyo imebaini pia kuwa washambuliaji kadhaa waliuawa wakati wa mapigano hayo, lakini haikubainisha idadi yao.

Baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali mwaka jana huku wakijiandaa pia kuondoka Burkina Faso, Ufaransa itapeleka wanajeshi 3,000 pekee katika eneo lenye machafuko la Sahel katika nchi za Niger  na Chad, kunakoripotiwa makundi ya kigaidi.