1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Walinda amani UN waanza kuondoka DR Kongo

Iddi Ssessanga
29 Februari 2024

Umoja wa Mataifa umeanza kuondoa askari wa kulinda amani kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya Jumatano, na hivyo kuhitimisha uwepo wa miaka 25 huku mzozo ukiongezeka mashariki mwa taifa hilo la Afrika.

https://p.dw.com/p/4d0f0
DR Kongo MONUSCO
MONUSCO imekuwepo DR Kongo kwa zaidi ya miaka 25.Picha: MONUSCO/Xinhua/picture alliance

DR Congo ilidai kuondolewa kwa wanajeshi 13,500 waliosalia na polisi 2,000 katika mikoa inayopakana na Rwanda na Burundi licha ya wasiwasi wa kimataifa juu ya kukithiri kwa ghasia.

Katika hafla rasmi katika kambi ya Kamanyola katika jimbo la Kivu Kusini, ya kwanza kukabidhiwa, bendera za Umoja wa Mataifa na askari wa kulinda amani wa Pakistan kwenye kambi hiyo, zilibadilishwa na zile za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Polisi wa kitaifa wamechukua hatua na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bintou Keita, alisema huo ndio utakuwa mfano wa kujiondoa katika kambi zote za Umoja wa Mataifa.

Mkuu wa MONUSCO Bintou Keita
Mkuu wa MONUSCO Bintou KeitaPicha: Bianca Otero/ZUMA Wire/IMAGO

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuleta Utulivu nchini DR Kongo, au MONUSCO, ulianzishwa mwaka 1999 kwa nia ya kusitisha vita vya pili vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambavyo vilivikutanisha vikosi vya ndani vinavyoungwa mkono na Angola, Namibia na Zimbabwe dhidi ya vikosi pinzani vinavyoungwa mkono na Uganda na Rwanda.

Soma pia: 2023: Mwaka wa changamoto kwa walinda amani wa UN Afrika

Katika kilele chake kulikuwa na wanajeshi 20,000 wa UN katika nchi hiyo kubwa. Zaidi ya walinda amani 270 wa MONUSCO wameuawa, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Kinshasa kwa muda mrefu imekuwa ikikishutumu kikosi cha Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kuwalinda raia dhidi ya makundi yenye silaha ambayo yamekuwa yakisumbua mashariki mwa nchi hiyo kwa miongo mitatu.

Mamia ya maelfu ya vifo vinaelezwa kusababishwa na mfululizo wa migogoro tangu miaka ya 1990. Takriban watu milioni sita wamekimbia makazi yao.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura mwezi Disemba kukubaliana na matakwa ya Kinshasa na kuanza kuzima taratibu kwa MONUSCO.

DR Kongo| Kijiji cha Blukwa katika mkoa wa Ituri
Raia wa Kongo wamekuwa wakiilamu MONUSCO kwa kushindwa kuwalinda dhidi ya makundi ya waasiPicha: Paul Lorgerie/DW

DR Congo ilidai kuondolewa kwa wanajeshi 13,500 waliosalia na polisi 2,000 katika mikoa inayopakana na Rwanda na Burundi licha ya wasiwasi wa kimataifa juu ya kukithiri kwa ghasia.

Katika hafla rasmi katika kambi ya Kamanyola katika jimbo la Kivu Kusini, ya kwanza kukabidhiwa, bendera za Umoja wa Mataifa na askari wa kulinda amani wa Pakistan kwenye kambi hiyo, zilibadilishwa na zile za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Soma pia:UN yajiandaa kuanza kuondoa walinda amani DR Kongo

Polisi wa kitaifa wamechukua hatua na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bintou Keita, alisema huo ndio utakuwa mfano wa kujiondoa katika kambi zote za Umoja wa Mataifa.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuleta Utulivu nchini DR Kongo, au MONUSCO, ulianzishwa mwaka 1999 kwa nia ya kusitisha vita vya pili vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambavyo vilivikutanisha vikosi vya ndani vinavyoungwa mkono na Angola, Namibia na Zimbabwe dhidi ya vikosi pinzani vinavyoungwa mkono na Uganda na Rwanda.

DW Kongo Kivu Kaskazini| Maandamano dhidi ya MONUSCO
Maandamano yamekuwa yakifanyika mara kwa mara kupinga uwepo wa MONUSCO DR Kongo.Picha: Benjamin Kasembe/DW

Katika kilele chake kulikuwa na wanajeshi 20,000 wa UN katika nchi hiyo kubwa. Zaidi ya walinda amani 270 wa MONUSCO wameuawa, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Kinshasa kwa muda mrefu imekuwa ikikishutumu kikosi cha Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kuwalinda raia dhidi ya makundi yenye silaha ambayo yamekuwa yakisumbua mashariki mwa nchi hiyo kwa miongo mitatu.

Mamia ya maelfu ya vifo vinaelezwa kusababishwa na mfululizo wa migogoro tangu miaka ya 1990. Takriban watu milioni sita wamekimbia makazi yao.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura mwezi Disemba kukubaliana na matakwa ya Kinshasa na kuanza kufungwa taratibu kwa shughuli za MONUSCO.

Waziri wa mambo ya nje Christophe Lutundula amesema anataka uondoaji huo ukamilike mwishoni mwa mwaka huu, ingawa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halijaweka tarehe.

Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DR Congo waliwaua kwa njia ya umeme waandamanaji 4 kwa bahati mbaya.
Maandamano dhidi ya MONUSCO wakati mwingine yaligeuka kuwa ya maafa.Picha: Stringer/AA/picture alliance

Wanajeshi hao wako katika majimbo ya Ituri, Kivu Kusini na Kivu Kaskazini ambayo yameathirika zaidi kwa miongo kadhaa. Kuondoka kwa MONUSCO kutafanyika katika awamu tatu.

Awamu ya kwanza itashuhudia kuondoka kwa walinda amani kutoka vituo 14 vya Kivu Kusini mwishoni mwa Aprili. Kivu Kaskazini na Ituri zitafuata.

Ni "wakati wa kihistoria", kamanda mkuu wa MONUSCO Jenerali Diouf Khar alisema katika hotuba yake.

"Tulianza na Kamanyola kwa sababu kuna utulivu hapa ambao unatuwezesha kuondoka," Keita aliwaambia waandishi wa habari.

Hisia mchanganyiko kuhusu uondokaji wa MONUSCO

Huko Kamanyola, yenye wakazi wapatao 100,000, maoni yalionekana kugawanyika kuhusu kujiondoa. Ombeni Ntaboba, mkuu wa baraza la vijana eneo hilo, alisema hana wasiwasi.

Kila jioni, alisema, "tunawaona wakiwa kwenye magari yao ya kivita karibu na uwanda wa Ruzizi", ambapo makundi yenye silaha yanafanya kazi mpakani.

"Lakini kiwango cha ukosefu wa usalama bado ni kile kile, pamoja na ujambazi wa kutumia silaha na utekaji nyara."

"Tunapongeza uamuzi wa serikali ya Kongo," alisema Mibonda Shingire, mwanaharakati wa haki, ambaye hata hivyo alikiri kuhofia athari za uchumi kutokana na ukweli kwamba MONUSCO inaajiri raia wengi.

Wengine, kama Joe Wendo, walisema walikuwa na wasiwasi kuhusu "ombwe la kiusalama" baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Pakistani. "Uwepo wao angalau ulitulinda dhidi ya wavamizi wa Rwanda," alisema.

Wakaazi Kivu washinikiza kuondolewa MONUSCO DRC

Kitisho cha waasi wa M23

Waasi wa M23 wanaoongozwa na Watutsi wameteka maeneo mengi katika eneo jirani la Kivu Kaskazini. Mapigano makali yalianza tena mwezi uliopita karibu na Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini.

Kinshasa, Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi zinasema Rwanda inawaunga mkono M23 katika jitihada za kudhibiti rasilimali kubwa ya madini katika eneo hilo. Rwanda inakanusha kuwa na jukumu lolote. Wananchi wa eneo hilo pia wamewakosoa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.

Soma pia: Wanajeshi wa Monusco kuondoka Kongo ifikapo Disemba

Na uongozi wa MONUSCO hivi karibuni ulilazimika kuangazia jukumu lake la "kuunga mkono vikosi vya jeshi vya Kongo ... kutetea maeneo yake ... kuwezesha njia salama kwa raia".

"Kuondoka kwa helmeti za bluu za MONUSCO kunatuhusu, wakati ambapo nchi iko vitani na waasi wanaoungwa mkono na majirani zetu wa Rwanda," alisema Beatrice Tubatunziye, ambaye anaongoza chama cha maendeleo huko Kamanyola.

Alisema watu walikuwa wakitegemea majeshi ya Kongo "kuwa na uwezo wa haraka wa kujaza pengo".      

Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa vikosi vya usalama vya DR Congo lazima viimarishwe na kuwatunza raia wakati huo huo MONUSCO ikijiondoa.