1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wadau wa afya Afrika Mashariki wakutana Arusha

Veronica Natalis
20 Januari 2023

Wadau wapatao 100 wa masuala ya afya kutoka nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki, wamekutana katika makao makuu ya jumuiya hiyo yaliyopo Arusha Tanzania, kujadili mipango ya utekelezaji wa afya ya pamoja.

https://p.dw.com/p/4MUhB
Kenia | Impfung gegen Malaria
Picha: Joseph Oduor/AP Photo/picture alliance

Wadau hao wa afya pia wanakutana hapa kubainisha mikakati ya kuzuia magonjwa ya milipuo. Kwa miongo miwili iliyopita Jumuiya ya afrika Mashariki imekumbwa na magonjwa ya kuvuka mpaka na kushuhudia athari zake katika sekta nyingi zikiwepo ya uchumi na biashara. 

Huu unakuwa mkutano wa kwanza wa mwaka wa wadau wa sekta ya afya kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki na unafuatia mapendekezo ya timu ya wataalamu kutoka jumuiya hiyo  yaliyotolewa mwezi Novemba mwaka 2021 na hivyo jumuiya imeandaa mkutano huo kwa lengo la kupanga utekelezaji wa pamoja wa mikakati kuhusu kushughulika na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza miongoni mwa nchi wanachama.

Soma Zaidi: Kila Mkenya aliyetimiza miaka 18 kulipia bima ya afya

Dkt Irene Isaka ni mkurugenzi wa sekta za jamii kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na mambo mengine anasema mkutano huu unaweka alama ya kuwa ni mwanzo wa ushirikiano wa pamoja wa kushughulika na magonjwa ya milipuko. "Ushiriki wenu mzuri katika jukwaa hili la kwanza la wadau wa afya ya pamoja kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki, kunaonesha dhamira ya dhati ya kushirikiana katika kuzuia na kukabiliana na magongwa ya milipuko ya magonjwa katika ukanda wetu. Na huu ni msingi bora wa ushirikiano utakaoendelea kila mwaka katika siku zijazo.” amesema Dr. Isaka.

Tansania Muhimbili National Hospital in Daressalam
mafunzo ya utoaji wa huduma za afya kwa vitendo pia ni muhimu katika kuimarisha sekta ya afya.Picha: DW/R. Velton

Mipango ya mikakati ya utekelezaji wa afya ya pamoja, ni ya kuanzia mwaka  2022-2027, Kupitia mpango wa kimataifa wa kuzuia na kukabili magonjwa ya milipuko, afya kwa pamoja, itakuchunguza na kukuza mawasiliano baina ya wataalamu wa afya ya binadamu, Wanyama na mazingira, ili kudhibiti majanga ya magonjwa miongoni mwa nchi wanachama kufuatia kushuhudiwa magonjwa ya milipuko kama Ebola, Virusi vya Corona na kipindupindu katika baadhi ya nchi.

Godje Bialluch ni mratibu wa GIZ Afrika Mashariki. "Jumuiya ya Afrika Mashariki imekumbwa na milipuko kadhaa ya magonjwa ya kuambukiza yanayoibuka mara kwa mara katika miongo miwili iliyopita. Hii imekuwa na athari mbaya sio tu kwa afya za watu na Wanyama lakini pia athari zake zimeonekana katika biashara, elimu, utalii na uchumi kwa ujumla."

Soma Zaidi:Ubadhirifu wa huduma za dawa katika hospitali za mikoa Tanzania 

Pamoja na mambo mengine mkutano  huo wa wadau  wa afya ambao umefadhiliwa na shirika la misaada la Ujerumani GIZ, umeongeza uelewa na kubadilishana uzoefu pamoja na kuweka mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja.