1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Upinzani Tunisia wasema polisi walijaribu kuzuia mkutano

9 Januari 2023

Muungano mkuu wa upinzani nchini Tunisia umeonya kwamba uhuru wa mikusanyiko na kujieleza uko hatarini baada ya polisi kujaribu kuzuia kufanyika kwa mkutano wa kisiasa dhidi ya Rais Kais Saied.

https://p.dw.com/p/4LvFU
Tunesien | Protest der Opposition gegen Präsident Kais Saied, in Tunis
Picha: Zoubeir Souissi/REUTERS

Muungano mkuu wa upinzani nchini Tunisia umeonya kwamba uhuru wa mikusanyiko na kujieleza uko hatarini baada ya polisi kujaribu kuzuia kufanyika kwa mkutano wa kisiasa dhidi ya Rais Kais Saied. Katika taarifa, muungano huo wa upinzani unaojumuisha chama cha Ennahdha, umesema unalaani uvamizi wa maafisa wa usalama wa Kais Saied na matumizi yao ya nguvu na matusi. Kulingana na taarifa hiyo, mkutano huo lakini uliendelea na kutoa wito wa Watunisia kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa Januari 14 katika maadhimisho ya rais wa zamani wa Tunisia Zine el-Abidine Ben Ali kwenda uhamishoni. Picha katika mitandao ya habari na mitandao ya kijamii katika taifa hilo la kaskazini mwa Afrika zimeonyesha polisi wakijaribu kuzuia kufanyika kwa mkutano huo wa kisiasa katika mitaa ya Mnihla huko Tunis.