1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Umoja wa Mataifa wasema idadi ya vifo yaongezeka Haiti

Tatu Karema
20 Aprili 2024

Zaidi ya watu 2,500 waliuawa au kujeruhiwa katika ghasia za magenge nchini Haiti kuanzia mwezi Januari hadi Machi, hili likiwa ongezeko la asilimia 53 kutoka miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2023.

https://p.dw.com/p/4f0Ld
Maafisa wa polisi washika doria mjini Port-Au-Prince, Jumatatu Aprili 8,2024
Maafisa wa polisi washika doria mjini Port-Au-PrincePicha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance

Ripoti ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Haiti, BINUH imeelezea hali hiyo ya Haiti hapo jana.

Ripoti hiyo inasema kuwa takribani watu 590 waliuawa wakati wa operesheni za polisi. Wengi wa watu hao hawakuhusika na vurugu za magenge,  baadhi walikuwa walemavu, huku wengine 141 wakiuawa na makundi yenye silaha.
Soma pia:Mamia ya mashirika yaiomba Marekani kutowarejesha raia wa Haiti wanaokimbia machafuko

Ghasia nyingi zilitokea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Port-au-Prince, huku takriban watu 438 wakitekwa nyara katika eneo la Artibonite.

Wafuasi wa magenge waliwabaka wanawake na wasichana

Ripoti hiyo imeongeza kuwa wafuasi wa magenge hayo walifanya ubakaji dhidi ya wanawake na wasichana katika maeneo ya wapinzani wao pamoja na magerezani na kambi za wakimbizi.