1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulimwengu waadhimisha Siku ya Chakula bila chakula

16 Oktoba 2023

Ulimwengu unaadhimisha leo Siku ya Chakula Duniani ambapo kumekuwepo wito wa kimataifa wa kuchukuwa hatua za kuhakikisha upatikanaji wa chakula na maji, ambazo huduma muhimu kwa mwanaadamu.

https://p.dw.com/p/4Xabt
Uganda Amudat | Frauen bei Ernte von Feldfrüchten
Wanawake wa Uganda wakivuna mboga.Picha: LUIS TATO/FAO/AFP

Sherehe za kuadhimisha siku hiyo zimefanyika katika makao makuu ya Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) mjini Roma na kuhudhuriwa na wageni maalum.

Soma zaidi: Je zitarajiwe ahadi mpya kupambana na njaa duniani?

"Vita vinaendelea Mashariki ya Kati lakini pia Ulaya kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Vita huchangia kuongezeka kwa ukosefu wa utulivu katika maeneo mbalimbali ya dunia, hasa katika nchi zilizo hatarini zaidi, na hivyo kuzidisha uhaba wa chakula na uhaba wa bidhaa muhimu. Haki ya chakula na maji inajumuishwa katika haki ya kuishi. Hiyo ni changamoto inayohitaji ushirikiano." Alisema Rais Sergio Mattarella wa Italia akihutubia mkutano huo.

 Viongozi wengine waliohudhuria sherehe hizo ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Mfalme Letsie III wa Lesotho.