1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yapambana kurudisha umeme baada ya mashambulizi

6 Desemba 2022

Ukraine inapambana kurudisha umeme baada ya wimbi la hivi karibuni la mashambilizi ya Urusi kusababisha athari ya kukatika kwa umeme katika maeneo mengi ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4KWvW
BdTD | Ukraine-Krieg Irpin | Bewohner kochen im Freien
Picha: DIMITAR DILKOFF/AFP

Rais Volodymyr Zelensky amesema kati ya makombora 70 yaliyorushwa na Urusi mengi yalidunguliwa ingawa bado miundo mbinu ya nchi yake iliathirika kwenye matukio hayo.

Shirika la usambazaji umeme Ukraine, Ukrenegro limesema hatua mpya ya kuzimwa umeme imetangazwa katika maeneo yote ya nchi kutokana na athari zilizosababishwa na mashambulizi.

Hali hiyo inashuhudiwa wakati viwango vya joto vinateremka na baridi imeanza kuongezeka nchini Ukraine.

Rais Zelensky amesema wakati Urusi iliuchagua kufanya mashambulizi hayo unafungamana na nia ya nchi hiyo ya kutaka kusababisha uharibifu mkubwa kadri inavyoweza. Takriban nusu ya mfumo mzima wa nishati nchini Ukraine imeshaharibiwa.