1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yadungua ndege 27 za Urusi zisizoendeshwa na rubani

Josephat Charo
10 Oktoba 2023

Jeshi la anga la Ukraine limesema limeziharibu ndege 27 kati ya 36 za Urusi zinazoendeshwa bila rubani usiku wa kuamkia leo kusini mwa nchi.

https://p.dw.com/p/4XLHr
Ukraine limesema ndege hizo zilizotengenezwa nchini Iran chapa Shahed-136/131
Ukraine limesema ndege hizo zilizotengenezwa nchini Iran chapa Shahed-136/131Picha: Evgeniy Maloletka/AP PHoto/picture alliance

Katika taarifa yake iliyoandikwa kwenye mtandao wa Telegram jeshi la Ukraine limesema ndege hizo zilizotengenezwa nchini Iran chapa Shahed-136/131 zilizorushwa na vikosi vya Urusi kutokea eneo la Crimea zilitunguliwa na kuharibiwa na mifumo ya ulinzi wa anga katika maeneo ya kusini ya Kherson, Mykolaiv na Odesa.

Gavana wa Odesa Oleh Kiper amesema miundo mbinu ya vifaa imeshambuliwa lakini hakuna watu waliojeruhiwa.

Wakati hayo yakiarifiwa, rais wa Ukraine Volodymir Zelensky yuko ziarani mjini Bucharest, Romania kwa mazungumzo kuhusu usalama.

Zelensky amesema atazungumza na rais Klau Iohannis na kuimarisha mahusiano baina ya nchi zao.