1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine inapania kuimarisha uwezo wake wa anga mwaka 2024

17 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba amesema leo kuwa kipaumbele cha nchi yake mwaka huu ni kuwa na udhibiti wa anga yake, katika wakati ambapo mashambulizi ya Urusi yanaingia mwaka wake wa tatu.

https://p.dw.com/p/4bM7K
Ukraine | Dmytro Kuleba
Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba Picha: Thomas Peter/REUTERS

Akihutubia kongamano la kiuchumi la dunia linalofanyika mjini Davos Uswisi, Kuleba ameeleza kuwa kipaumbele chao ni kuchukua udhibiti wa anga na kuiangusha Urusi. 

Amesema kuwa, yeyote anayedhibiti anga ndiye atakayeamua muelekeo wa vita hivyo.

Kauli yake inafanana na ile iliyotolewa jana na Rais Volodymyr Zelenksy aliyesema kuwa, lazima Ukraine "iimarishe ulinzi wake wa anga" ili kuipa mafanikio katika mapambano ya ardhini.

Kwa muda mrefu, Ukraine imewatolea mwito washirika wao wa Magharibi kuipa ndege za kivita za kisasa ili kuwasaidia wanajeshi wake wanaopambana na vikosi vya Urusi kusini na mashariki wa nchi hiyo.