1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Ujumbe wa UN watakiwa kumaliza shughuli zake Sudan

17 Novemba 2023

Utawala wa kijeshi Sudan umelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kusitisha mara moja majukumu ya Ujumbe wake nchini humo, ikiishutumu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake kama ilivyoainishwa. wake wa

https://p.dw.com/p/4Z2np
Sudan Khartum | Maandamano
Maandamano ya kupinga kile wasudan wanachosema ni kuingiliwa mambo yao ya ndani na mataifa ya kigeniPicha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limefanya mkutano wake na kupokea ripoti kuhusu hali ya mambo nchini Sudan ilioandaliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNITAMS. Sudan ilitumia jukwaa hilo kuwasilisha barua ilioelekezwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambapo mbali na mambo mengine uliitaka Ujumbe huo kuondoka nchini humo kwa kile ilichokisema kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Kaimu waziri wa mambo ya nchi za nje wa Sudan, Ali Sadeq, aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, dhamira ya Sudan na kuwahakikishia kwamba serikali yake imejitolea kushirikiana na Umoja huo katika mwelekeo chanya na salama.

UN: Nusu ya raia wa Sudan wanahitaji msaada wa kiutu

Al-Harith Idriss  Mohamed, Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa, Sudan alisema hayo ni maamuzi ya Sudan baada ya kutathmini kile kinachoendelea kwa sasa nchini mwake.

"Ningependa kuwasilisha maamuzi ya serikali ya Sudan kwamba Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unapaswa kuondoka mara moja, hii ni kutokana na barua iliowasilishwa kwa Katibu Mkuu Antonio Guterres," alisema Al Harith.

Aliongeza kuwa madhumuni ya kupelekwa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo ni kuisaidia serikali ya mpito ya Sudan baada ya mapinduzi ya Desemba 2018," lakini utendaji wa ujumbe huo katika kutekeleza malengo yake "ulikuwa wa kukatisha tamaa."

Hali ya Uhasama Sudan yaongezeka

Hata hivyo Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa umeliambia Baraza la Usalama kuwa hali ya uhasama nchini Sudan imeongezeka katika siku za hivi karibuni na hakuna dalili za kupungua.

Katibu Mkuu Msaidizi wa Afrika Martha Ama Akyaa Pobee, amesema wakati pande mbili zinazohasimiana zikitangaza kujadili utayari wa kusitisha mapigano, hatua zao kwa msingi zinaonyesha vinginevyo na kuitaka jumuiya ya kimataifa irejeshe dhamira yake ya kufufua juhudi za pamoja za amani kwa kuzingatia athari zinazowakuta raia kwa sasa. 

Umoja wa Ulaya washutushwa na mauaji ya raia 1,000 Darfur

"Kwa kuzingatia hali iliyobadilika sana tangu kuzuka kwa mzozo huo, Katibu Mkuu ameanzisha mapitio ya kimkakati ya UNITAMS ili kulipatia Baraza hili chaguzi za jinsi ya kurekebisha majukumu ya Ujumbe ili kuendana vyema na muktadha wa sasa. Hii itasaidia kuhakikisha kwamba malengo na vipaumbele vya Ujumbe huo vinaakisi ipasavyo mahitaji ya watu wa Sudan na kusaidia Sudan katika njia yake ya kuelekea amani na utulivu," alisema Pobee.

Mazungumzo ya kutafuta amani Sudan yakwama

Mnamo mwezi April vita kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF baada ya wiki kadhaa za mvutano ulioongezeka kati ya pande hizo mbili kuhusu mpango wa kuunganisha vikosi kama sehemu ya mpito katika utawala wa kijeshi.

afp,reuters