1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Italia kufanya mkutano wa kilele Berlin

22 Novemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni leo watakubaliana kushirikiana katika masuala ya nishati hadi ulinzi katika mkutano wa kilele utakaofanyika mjini Berlin.

https://p.dw.com/p/4ZIr1
Diplomasia | Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Waziri Mkuu Italia Giorgia Meloni
Ushirikiano | Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Waziri Mkuu Italia Giorgia MeloniPicha: Roberto Monaldo/LaPresse via AP/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni leo watakubaliana kushirikiana katika masuala ya nishati hadi ulinzi katika mkutano wa kilele utakaofanyika mjini Berlin.

Mkutano huo ndio wa kwanza kufanyika baina ya nchi hizo katika kipindi cha miaka saba. Mpango wa utendajiwa kurasa 31 utakaotiwa saini na viongozi hao wawili katika mkutano huo na ambao shirika la habari la Reuters limeona nakala yake, haujalipa kipau mbele suala la uhamiaji, licha ya kuwa mpango wa uhamiaji wa Ujerumani unaoana na ule wa Italia.

Soma pia:Nigeria na Ujerumani zatia saini makubaliano ya gesi na nishati mbadala

Katika mpango huo Ujerumani na Italia zinaahidi kuwa na majadiliano ya mara kwa mara, kwa mfano kupitia mikutano ya mawaziri wake wa ulinzi na mambo ya nje na kushirikiana kwa karibu katika sera muhimu. Mkutano huo wa kilele leo utatanguliwa na mkutano wa kibiashara kati ya Ujerumani na Italia.