1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Uingereza ingali na lengo kuwapeleka wakimbizi Rwanda

18 Machi 2024

Uingereza bado yataka kuutimiza mpango wake wa kuwapeleka wakimbizi nchini Rwanda

https://p.dw.com/p/4drxa
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi SUnak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi SUnakPicha: Yui Mok/PA Wire/dpa/picture alliance

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesema Jumatatu kwamba bado serikali yake ina matarajio ya kuanza zoezi la kuwapeleka Rwanda wahamiaji wanaotafuta hifadhi nchini Uingereza.

Amesema zoezi hilo linatarajiwa kuanza wakati wa majira ya machipuo ambao utakwenda kulingana na ratiba ya awali ya mpango huo unaojadiliwa hivi sasa bungeni.

Sunak aliwaambia hayo waandishi wa habari wakati wa safari yake katika mji wa Coventry katikati mwa Uingereza.

Waziri Mkuu wa Uingereza amesema ni muhimu kuufanikisha mpango huo wa kuwapeleka wakimbizi nchini Rwanda kwa sababu nchi yake inahitaji kuweka vizuizi kwawahamiaji wanaongia Uingereza kinyume cha sheria.