1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tuchel: Tuko pazuri kuelekea mechi za kimataifa

9 Oktoba 2023

Mabingwa Bayern Munich waliridhika na ushindi wa 3-0 walipokuwa wakichuana na Freiburg ingawa mshambuliaji wao Harry Kane, hakuweza kuzitumia vyema nafasi alizopata na kuwa miongoni mwa wafungaji katika mechi hiyo.

https://p.dw.com/p/4XJJg
Ligi Kuu ya Ujerumani, RB Leipzig - Bayern München
Kocha wa Bayern Munich Thomas TuchelPicha: Hendrik Schmidt/dpa/picture alliance

Kocha Thomas Tuchel lakini amesema matokeo hayo ndio waliyokuwa wanayahitaji kabla mapumziko ya mechi za kimataifa.

"Tulistahili kuyapata matokeo haya, kusema kweli mabao yangekuwa mengi zaidi kwa kuwa tulibuni nafasi nyingi. Nimeridhishwa na jinsi tulivyocheza nafurahi na matokeo yalikuja yenyewe tu. Ni mwisho mwema wa kipindi hiki," alisema Tuchel.