1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yataka ujumbe wa kulinda amani uondolewe mara moja

John Juma
17 Novemba 2023

Sudan imetoa wito wa kuondolewa kwa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa UNITAMS katika taifa hilo la pembe ya Afrika. Lakini serikali ya kijeshi ya Sudan imesema imejitolea kushirikiana na Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/4Z1qI
Sudan maandamano
Maandamano dhidi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa SudanPicha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Kupitia barua waliyomuandikia Katibu Mkuu wa umoja wa huo Antonio Guterres, na pia katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kaimu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Ali Sadeq, ametaka Ujumbe Jumuishi wa Usaidizi wa Mpito nchini Sudan (UNITAMS), uondolewe mara moja.

Sadeq amesema madhumuni ya kuanzisha misheni hiyo ilikuwa kusaidia serikali ya mpito ya Sudan baada ya mapinduzi ya Desemba 2018 na kuongeza kuwa utendakazi wa ujumbe huo katika kutekeleza malengo yake ni wa kukatisha tamaa.

Ujumbe huo una zaidi ya wafanyikazi 400 wengi wao wakiwa ni raia.