1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaChina

Watu 11 wamekufa kufuatia maporomoko ya ardhi Yunnan, China

23 Januari 2024

Timu ya uokoaji inaendelea kutafuta manusura zaidi baada ya kutokea maporomoko ya ardhi katika wilaya ya Yunnan, kusini magharibi mwa China.

https://p.dw.com/p/4bZSH
Timu ya waokoaji inaendelea kutafuta manusura baada ya kutokea maporomoko ya ardhi katika kijiji cha Liangshui, China
Timu ya waokoaji inaendelea kutafuta manusura baada ya kutokea maporomoko ya ardhi katika kijiji cha Liangshui, ChinaPicha: Zhou Lei/Xinhua/picture alliance

Watu 11 wamekufa na wengine 47 wamenasa chini ya vifusi kufuatia maporomoko hayo ya ardhi yalitokea usiku wa kuamkia leo.

Rais wa China Xi Jinping ameagiza nguvu zote zielekezwe katika kutafuta manusura.

Vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kuwa, uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa maporomoko hayo ya ardhi yalisababishwa na kuanguka kwa mwamba.

Zaidi ya watu 500 wamehamishwa kutoka majumbani mwao huku timu ya waokoaji 1,000 wakitumwa katika eneo la mkasa. Naibu Waziri Mkuu Zhang Guoqing anaripotiwa kuongoza timu ya waokoaji katika eneo la mkasa.

China imekumbwa na msururu wa majanga katika miezi ya hivi karibuni ikiwemo mvua kubwa za ghafla na baridi kali.